Kuanzia tarehe 6 hadi 9 Mei, 2024, Shirika la CRC lilikuwa miongoni mwa asasi zilizoshiriki katika warsha maalum iliyoandaliwa mkoani Kilimanjaro na Mtandao wa Kutokomeza Ndoa za Utotoni (TECMN). Lengo kuu la warsha hiyo lilikuwa kujifunza na kushirikiana kutengeneza Mpango Kazi wa miaka mitatu wenye malengo ya dhati ya kutokomeza ndoa za utotoni nchini Tanzania.

Warsha hiyo iliandaliwa kwa kushirikisha wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia, mashirika ya kimataifa, na serikali, ili kujadili mbinu bora za kukabiliana na tatizo la ndoa za utotoni, ambalo linaathiri maelfu ya wasichana kila mwaka. Mpango Kazi huo unatarajiwa kuboresha uratibu wa juhudi za kuzuia ndoa za utotoni na kusaidia kuongeza uelewa wa haki za watoto, hasa wasichana.

Kupitia ushirikiano wa wadau, warsha hiyo imewezesha kubuni mikakati inayozingatia elimu, ulinzi wa watoto, na ushirikiano na jamii ili kufikia lengo hili muhimu la kijamii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *