Tarehe 16 na 17 Mei, 2024, Shirika la CRC liliandaa majadiliano muhimu na Wabunge wa Bunge la Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wa dini na wa kimila. Majadiliano hayo yalilenga kujadili suala zima la uzazi salama kwa vijana wa Tanzania, hususan kundi rika.

Vikao hivyo vilifanyika mkoani Dodoma na vilihudhuriwa na wadau mbalimbali wenye ushawishi katika jamii na ngazi za kisiasa. Lengo kuu lilikuwa kujenga uelewa na kuimarisha mikakati ya kuhakikisha vijana wanapata elimu sahihi na huduma za uzazi salama. Viongozi wa dini na wa kimila walishirikiana kwa karibu na wabunge ili kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili vijana katika masuala ya afya ya uzazi.