Tarehe 12 Septemba, 2024, Kituo cha Usuluhishi (CRC) kilishiriki Mkutano Mkuu wa Watetezi wa Haki za Binadamu uliofanyika mjini Arusha. Aidha, CRC ilipata fursa ya kushiriki katika Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) tarehe 12-13 Septemba, 2024.

Kupitia mikutano hii, CRC imeongeza uelewa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku, hasa katika masuala yanayohusu utetezi wa haki za binadamu na ushirikiano na wadau mbalimbali.