Shirika la WiLDAF limeandaa mafunzo ya siku tatu kwa wawezeshaji wa mafunzo ya uongozi, yaliyoelekezwa kwa wanawake wana siasa wanaotarajia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Katika mafunzo haya, Kituo cha Usuluhishi (CRC) kimeshiriki kikamilifu katika kuandaa vitini vya mafunzo pamoja na kushiriki kwenye mafunzo hayo.

Lengo la mafunzo haya ni kuwawezesha wanawake wanaotarajia kugombea nafasi za uongozi kwa kuwapatia ujuzi, mbinu, na maarifa ya uongozi, ili kuongeza uwakilishi wa wanawake katika ngazi za maamuzi na uongozi.