
Kituo cha Usuluhishi (CRC) kimeshiriki mafunzo ya siku mbili kuhusu haki na utetezi wa watoto, yaliyoendeshwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC). Mafunzo haya yalifanyika kwa kushirikiana na Law School ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), East Africa Human Rights Institute, na Tanzania Child Reform Forum (TCRF).
Mafunzo haya yalilenga kuwajengea uwezo washiriki katika kushughulikia changamoto zinazowakabili watoto nchini Tanzania, pamoja na kuboresha mbinu za kutetea haki zao katika ngazi mbalimbali za kijamii na kisheria.

